Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCO Bwa. John J. Kyaruzi akisaini makubaliano hayo na Mwasisi wa Shirika la Bothar Bwa. Peter Ireton huku wakishuhudiwa na Dkt. Bernard Muyeya (kulia) Mkurugenzi wa Huduma za Nje ya Nchi wa Bothar na Bwa. Abdallah S. Msambachi ( kushoto) Mratibu wa Biashara wa Mfuko wa SAGCOT. 

Ikiwa
ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza tija na uzalishaji kwa
wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe, Iringa na Mbeya, Mfuko
Kichocheo wa SAGCOT yaani SAGCOT CATALYTIC TRUST FUND tarehe 12 Agosti
2016 umesaini makubaliano na Shirika la Bothar kutoka nchini Ireland
ambalo linajihusisha na kutoa misaada mbalimbali inayolenga kutoa fursa
kwa familia zenye kipato cha chini kuweza kuboresha maisha yao kupitia
uwekezaji wa shughuli zinazowaletea kipato hususani kaya
zinazojishughulisha na ufugaji.

Katika makubaliano hayo jumla ya
Ng’ombe wa kisasa 630 wanatarajiwa kuingizwa nchini katika kipindi cha
miaka mitatu. Ng’ombe hao watagawiwa kwa wafugaji walioandaliwa chini ya
miradi inayotekelezwa na Mfuko huo, Aidha wafugaji watahakikishiwa
masoko pamoja na huduma mbalimbali za mifugo kupitia wataaalamu wa
Halmashauri husika.

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT Bwa. John. J. Kyaruzi ( kushoto) akisaini makubaliano na Muasisi wa Bothar Bwa. Peter Ireton .
Bwa. John. J. Kyaruzi na Bwa. Peter Ireton wakibadilishana hati za makubaliano.
Mkurugenzi wa huduma za nje ya Nchi wa Bothar,Dkt Bernard Muyeya akitoa maelezo kwa wajumbe namna shirika hilo linavyotoa huduma zake.