ABIRIA wanaotumia usafiri wa treni inayofanya safari kati ya Stesheni, Dar es Salaam na Pugu, wataanza kulipa nauli ya Sh 600 baada ya nauli hiyo kupitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).
Awali treni hiyo ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ilikuwa ikitoza Sh 400 kwa mtu mzima na mwanafunzi Sh 200 wakati treni hiyo ilipokuwa katika majaribio.

Wanafunzi watalipa Sh 100 kutoka kituo kimoja hadi kingine.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Ng’hwani Rashid amesema, kampuni hiyo ilikuwa ikitoza Sh 400 wakati ikisubiri kukamilika kwa mchakato wa ukokotoaji nauli ambao umesimamiwa na Sumatra.
Kwa habari zaidi soma Maganga One Blog kila siku.