Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Aug 30, 2016

UVCCM wasitisha maandamano

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umetangaza kusitisha maandamano waliyokuwa wamepanga kuyafanya leo ili kuunga mkono juhudi na kazi inayofanywa na Rais John Magufuli, ikielezwa ni kutokana na kutii katazo la Jeshi la Polisi nchini.

Umesema kwamba umepokea majibu ya barua yao kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu inayowataka kuacha kufanya maandamano yao kwa sababu polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na maandamano nchi nzima.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wake, Shaka Hamdu Shaka, ilisema mbali na barua hiyo pia wamefikia uamuzi huo unatokana na utii, nidhamu na kuzingatia utaratibu wa mamlaka za juu ndani ya chama.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP