Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Aug 25, 2016

TLP yataka SMZ imtenge Maalim Seif

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
CHAMA cha Tanzania Labour(TLP) kimemuandikia barua Rais wa Mapinduzi wa Zanzibar, Dk Mohamed Ali Shein na kumtaka kuanzia sasa wamtenge Katibu Mkuu wa CUF , Maalim Seif Sharif Hamad (pichani), kwa kutomualika kwenye shughuli zozote za kitaifa mpaka atakapojirekebisha na kuitambua rasmi serikali iliyopo madarakani.

Aidha, kwa kuwa CUF inadai kwamba haiitambui serikali hiyo basi ruzuku kwa chama hicho isitishwe kuanzia sasa hadi hapo chama hicho kitakapoitambua rasmi serikali hiyo na kuacha kuhamasisha wananchi wasilipe kodi.
Katika barua ya chama hicho iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Augustine Mrema ilisema chama hicho kimesikitishwa na wanalaani kitendo kilichofanywa Hamad ambaye pia alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais kwenye serikali ya Umoja wa kitaifa wa Zanzibar (SUK) wakati wa maziko ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, marehemu Mzee Aboud Jumbe cha kukataa kumpa Rais Shein mkono wa kusalimiana.
Alisema kuleta tofauti za kisiasa msibani kwa makusudi, Maalim Seif ameendelea kuwagawa Wazanzibari kisiasa na kushindwa kumuenzi marehemu Aboud Jumbe, ambaye pamoja na kuiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu pia ndiye aliyemlea Maalim Seif kisiasa.
Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa marudio uliosusiwa na CUF, Maalim Seif amekuwa akileta chokochoko na uchochezi dhidi ya serikali ya Zanzibar akidai kwamba haitambui na kuwataka wananchi wa Zanzibar kugoma na kuwataka wasilipe kodi kwa serikali.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP