Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Aug 15, 2016

USAIN BOLT AENDELEA KUIDHIHIRISHIA DUNIA KUWA HANA MPINZA KWENYE KUKIMBIA

 Asubuhi ya kuamkia leo huko Rio De Janeiro nchini Brazil katika michuano ya Olympic, mwanariadha Mjamaica, Usain Bolt ameweza kupata ushindi tena wa pekee kwa kujipatia medali ya dhahabu kwa kukimbia mbio za mita 100 kwa sekunde 9.81.
Bolt ameweza kumpiku mpinzani wake Justin Gatlin mwenye asili ya America ambaye yeye amekimbia kwa sekunde 9.89 na kunyakua  medali ya Silver na mshindi wa tatu Andre de Grasse mwenye asili ya Canada akikimbia kwa sekunde 9.91.

Akiwa amejizatiti kuendelea kuweka rekodi, Bolt amebakisha michezo miwili ya mwisho ambayo atakimbia siku ya jumapili na kuweza kumaliza mashindano yake ya Olympic mwaka 2016

Mwaka 2012 katika michuano ya Olympic iliyofanyika nchini London katika mbio za Mita 100 na Mita 200 aliweza kushinda zote na kuondoka na Medali za dhahabu na Olympic ya mwaka 2008 iliyofanyika Beijing katika mfululizo huo huo wa mbio za mita 100 na 200 alifanikiwa kuchukua tena medali ya dhahabu.

Mkimbiza upepo huyo tangu aanze kushiriki Michuano ya Olympic mwaka 2008 hajawahi kushinda medali tofauti na dhahabu


Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP