Polisi nchini Zambia wamewakamata watu 133 wanaopinga kuchaguliwa tena kwa rais Edgar Lungu, baada ya mshindani wake mkuu Hakainde Hichilema kudai kuwa kura ziliibwa.
Maandamano yalizuka katika sehemu nyingi za mkoa wa Kusini ukiwemo mji maaarufu wa utalii wa Livingstone.

Mkuu wa Polisi Godwin Phiri, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa waandamanaji walikuwa wakiwalenga wafuasi wa chama tawala na kisha kuharibu mali yao.
Bwana Hichilema anasema kuwa ana mpango wa kupeleka kesi mahakamani kupinga matokeo.
Bwana Lungu alitangazwa mshindi na asilimia 50.35 kwenye uchaguzi huo wa siku ya Alhamisi huku Hichilema akipata asimia 47.67.