Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Sep 4, 2016

7,170 waliopita JKT waajiriwa

VIJANA 7,170 waliojiunga kwa kujitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wameajiriwa katika vyombo vya ulinzi na usalama kuanzia mwaka 2010 mpaka sasa.
Waziri wa Ulinzi na JKT, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema, kuanzia mwaka huo JKT huchukua vijana 5,000 hadi 7,000 kwa madhumuni ya kuwapa stadi za kazi na kuwajengea uzalendo.

Akizungumza katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na Televisheni ya Shirika la Utangazaji Taifa (TBC1), Dk Mwinyi alisema kuanzia mwaka 2010 vyombo vya ulinzi na usalama viliacha kuajiri kutoka uraiani, bali vijana waliopitia mafunzo hayo ambapo zaidi ya vijana 2,000 wamekuwa wakiajiriwa kwa mwaka.
Alisema pia kwa sasa kuna taasisi nyingi zimeanza kuchukua vijana waliopitia mafunzo hayo kama Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) na kampuni binafsi za ulinzi.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP