Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Sep 16, 2016

Hillary Clinton arejea kwenye mbio za kampeni baada ya kuugua

Mgombea Urais kupitia Chama cha Democratic nchini Marekani Bi Hillary Clinton amerejea kwenye mbio za kampeni baada ya kuugua homa ya mapafu.
Akiongea na mwandishi wa habari akiwa kwenye ndege kuelekea Greensboro North Carolina, Bi Clinton alisema anajiskia vizuri baada ya mapumziko ya siku tatu.
Mpinzani wake wa Chama cha Republican, Donald Trump ametoa barua kutoka kwa daktari wake ikionesha kuwa ana afya njema.
Barua hiyo inaonesha kuwa anatumia dawa ili kupunguza unene na kiwango kilichopitiliza cha uzito, lakini hatumii kilevi wala kuvuta sigara.

Trump aliwahi kuwa mchekeshaji wa vipindi vya runinga
Image captionTrump aliwahi kuwa mchekeshaji wa vipindi vya runinga

Uchaguzi wa Marekani utafanyika mwezi Novemba ambapo kampeni zake zimekuwa na vuta ni kuvute kutoka vyama vikubwa viwili vya Democratic na Republican.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP