Naibu Waziri wa TAMISEMI Sulemani Jafo akihutubia wadau wa kampeni ya kuchangia Madawati Mkoa wa Geita kwenye Harambee iliyofanyika Mjini Geita

    
Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila akitoa maelezo kuhusu namna Acacia ilivyoshiriki mwaka huu kuchangia kwenye zoezi la madawati.

      Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Bwana Graham Crew akiwa amenyoosha mikono kusalimia umma wa Watanzania waliongana kwenye harambee ya madawati Geita

Timu ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri baada ya Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila kutanga kuwa Mgodi utatoa shilingi milioni Mia Moja kwa ajili ya madawati Mkoa wa Geita.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.



Mgodi
wa Dhahabu Bulyanhulu  Umetoa Tsh 100m/- kwa Ajili ya Madawati ya Shule
Mkoani Geita. 




 Akitangaza
kiwango hicho katika hafla ya changizo iliyofanyika  Desire Park Mjini
Geita , Meneja Ufanisi na Mahusiano na Jamii wa Mgodi wa Dhahabu
Bulyanhulu bwana Elias Kasitila amesema, “Bulyanhulu  imebarikiwa
kuwa  karibu na Wilaya mbili,Halmashauri ya Msalala iliyopo Mkoa wa
Shinyanga na Nyang’wale iliyopo Mkoa wa Geita.


Hivyo basi tulipopokea  mwaliko kutoka  kwa Mkuu wa wilaya ya
Nyang’wale  kuhusu kampeni ya leo  ya madawati tumeamua kwamba
japokuwa  miradi mingine ya madawati tumeifanya mkoa wa Shinyanga tumeona
kuna umuhimu  wa kufanya hivyo  mkoa wa Geita pia.”alisema Kasitila.

"Hivyo
basi  siku ya leo tunajitolea  kuchangia Tsh100m/- kwa ajili ya
kampeni  za mikoa inayolenga kuondoa  upungufu wa  madawati
70,000.”aliongeza Kasitila.


 Elias
aliongeza kuwa, “misaada ya madawati kutoka kwenye migodi iliyoko chini
ya Acacia ambayo ni, North Mara, Buzwagi and Bulyanhulu,kwa mwaka huu Acacia
imetumia  takriban fedha za kitanzania zaidi ya Billion Moja  ambayo
inakadiliwa kutengeneza zaidi ya madawati 10,000.

 Mgeni
rasmi katika hafla ya kuchangia madawati mkoa wa Geita alikuwa Waziri Mkuu
wa  Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ambaye aliwakilishwa na Naibu Waziri
Ofisi ya Rais Tamisemi ,Utumishi na Utawala Bora, Mh.Suleiman Jafo.

 Akiwahutubia
washika dau waliokuwa  Desire park Naibu Waziri Jafo  alisema
“Nitapeleka salamu kwa waziri mkuu  kuhusiana na mwitikio ambao
nimeushuhudia leo  ninaagiza kamati ya Kampeni ya madawati Geita
kuorodhesha washika dau wote waliochangia  leo na kuwasilisha orodha hiyo
kwenye ofisi ya Waziri Mkuu ili binafsi awatambue wote walioonesha kuguswa
kuiondolea Geita uhaba wa madawati.”

 Katika
hafla hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Aacacia Bulyanhulu Graham Crew binafsi
alijitolea kuchangia  fedha za kitanzania shilingi 750,000/- kwa ajili ya
kampeni hiyo.