Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ,Bi Zainab Telack (aliye vaa ushungi) akiongozwa na Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii wa Mgodi
wa Dhahabu wa Bulyanhulu Elias Kasitila (kushoto kwake) wakati wakielekea uwanja wa Taifa wa mjini Kahama kwa ajili ya makabidhiano ya Madawati kutoka kampuni ya Acacia.
 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akihutubia wananchi
 katika uwanja wa Taifa Kahama wakati wa zoezi la Kukabidhiwa madawati
kutoka kwa kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Acacia, Bulyanhulu.


Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,kutoka kushoto ni Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi
wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Elias Kasitila, Afisa Miradi
Mzee Hamisi, Afisa Mahusiano ya Jamii William Bundala Chungu pamoja na Afisa
Mahusiano ya Jamii David Magege, wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama kabla ya zoezi la Kukabidhi
Madawati .
Baadhi ya waandishi wa habari wa  mkoa wa Shinyanga wakichukua taarifa kwa ajili ya kuuabarisha umma juu ya tukio la makabidhiano ya Madawati.
Madawati yaliyotolewa na kampuni ya Acacia kwa ajili ya shule katika mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi,Zainab Telack akikata utepe kuashiria kupokea madawati yaliyotolewa na kampuni ya Acacia.

Na Dixon Busagaga,Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack
amekabidhiwa madawati 2,000 yenye thamani ya Shilingi 240,800,000/= na Mgodi wa
Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya
Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Makabidhiano yamefanyika leo mjini Kahama.

Akimkabidhi madawati hayo Meneja wa Ufanisi wa
Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Bwana Elias Kasitila amesema, “hii ni awamu ya nne
kwa mgodi wa Acacia Bulyanhulu kukabidhi madawati ndani ya mwaka huu katika
kipindi ambacho taifa linaendelea kutekeleza kampeni ya kitaifa ya dawati kwa
kila mwanafunzi iliyoagizwa na Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr John Pombe Magufuli kwa lengo la kuboresha mazingira ya elimu nchini
Tanzania.”

Ameongeza kuwa, “licha ya Mgodi wa Dhahabu wa
Acacia Bulyanhulu kuchangia madawati pia inachangia miradi mingine kwenye jamii
lakini kwenye sekta ya elimu mgodi unashirikiana na jamii kuitekeleza miradi
kama vile ujenzi na ukarabati wa nyumba, ofisi za walimu madarasa, maabara za
sayansi na udhamini wa masomo kwa wanafunzi.”

Miradi ya Madawati 2016 kutoka Mgodi
wa Acacia Bulyanhulu

  • Mei tulikabidhi madawati 380 kwa Halmashauri ya Msalala yenye
    thamani ya shilingi  28,500,000/=
  • Juni tulikabidhi madawati 1,000 kwa Halmshauri ya Msalala
    yenye thamani ya shilingi 88,500,000/=
  • Julai tulikabidhi madawati 500 kwa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani
    Geita yenye thamani ya shilingi 37,500,000/=
  • Na hii leo Agosti tunakabidhi madawati 2,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa
    Shinyanga yenye thamani ya shilingi 240,800,000 /=
  • Aidha mwaka 2013 mgodi wa Acacia Bulyanhulu pia ulikabidhi dawati
    1,389 kwa Wilaya ya Kahama
Mchango wa Miradi ya Madawati Kwenye
Ajira
  • Katika kipindi cha miezi minne, utengenezaji wa madawati yenye
    thamani ya shilingi 393,800,000 umewezesha kutolewa kwa tenda za
    kutengeneza madawati kwa vikundi vya wajasiliamali wadogo na kuwawezesha
    vijana kujipatia ajira.
  •  
Wanafunzi ambao Wamenufaika
  • Mradi wa Madawati wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu umewaondelea adha
    jumla ya wanafunzi 5,040 ya kuketi sakafuni wakati wa kupokea  masomo
    yao, baada ya kupata madawati 3,880 bora ya kudumu ambayo yametengenezwa
    kwa awamu nne hadi sasa.
  •  
Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu
na Sekta ya Elimu Nchini
Mgodi wa Bulyanhulu unaamini kwamba elimu ni msingi
wa maendeleo ya jamii na unaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine
wa maendeleo katika ngazi mbalimbali kuendeleza shughuli za uboreshaji wa elimu
hapa nchini kupitia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na mgodi kupitia Mfuko wa
Maendeleo wa Kampuni ya ACACIA, (ACACIA Maendeleo Fund).

Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi Zainab Telack amesema, “ Tukio hili la
kukabidhiwa madawati ni tukio kubwa, nimefurahi sana na ninajua furaha ya
watoto watakaotumia madawati haya itakuwa mara mbili yake, kwa hivyo kwa niaba
ya Mkoa wa Shinyanga nawashukuru sana Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu kwa
kututengenezea madawati elfu mbili, mkoa wa Shinyanga ulikuwa na upungufu wa
Dawati elfu 7000 lakini sasa kupitia mchango wa leo kutoka Bulyanhulu na wadau
wengine sasa mkoa wetu unamaliza kabisa upungufu wa madawati.”