Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa katika makumbusho ya
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipotembele hivi karibu na kujifunza mambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya hayati baba wa taifa kwa ajili ya kuleta maendeleo ya nchi nzima

Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa katika kaburi la marehem
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere



Na fredy mgunda,musoma.

VIONGOZI wa vyama vya Siasa
wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa  aliokuwa nao
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake  ili
kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.






Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Bw. Haji Mnasi ambaye kitaaluma ni mwalimu mara baada  kutembelea Kaburi na Makumbusho ya Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo wilayani Butiama.



mimi kitaaluma ni mwalimu hivyo namuezi mwalimu kwa vitendo hata nilipokuwa afisa elimu iringa nilikuwa naingia darasani kufundi na sasa nitahakikisha nazilinda mali za taifa,nasisitiza uwajibika,uzalendo,uandilifu na nidhamu katika kulitumikia taifa la Tanzania kama unakumbuka mwalimu alikuwa anapenda kutumia neno (it can be done play your part) kila mtu atimizi majukumu yakeAmesema Mnasi.









Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa
Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya
kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa  vitendo hasa
uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo  na moyo wa kujitoa kwa dhati
kuwatumikia wananchi.









“Kupitia
kumbukumbu hizi sisi watumishi tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao
Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,  wengi wanadhani
Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu
watu wengine” Amesema Mnasi.









Ameeleza kuwa maisha aliyoishi Baba
wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale
alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya
madaraka na mali kwa  manufaa ya taifa.









“Sote ni mashahidi kupitia
kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu kabla hajajengewa nyumba
na Jeshi  kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika  eneo
lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu
aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Mnasi.









Bw. Mnasi
amebainisha kuwa  serikali itaendelea  kumuemzi Baba wa Taifa kwa
yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito
kwa  viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile
walivyonavyo.









“Suala la kuridhika na kuwa na kiasi
linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa  wanapaswa kuwaheshimu wananchi
wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali,  matokeo yanapotoka kama ni
sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao”  Ameainisha Mnasi.




Bw. Mnasi amemalizia kwa kuwataka watendaji wote wa serikali ya wilaya ya Ileje kufanya kazi kwa uaminifu,uadilifu,kuwajibika kwenye majukumu yao na kujituma na kamwe hata kuwa tayari kuwavumilia watendaji ambao ni wazembe kazini.









Kwa upande wake Mhifadhi wa
Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bw. Jacob Thomas
amesema kuwa  watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu
alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.









Amesema kuwa maisha ya uadilifu
aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania
na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.









“Ninyi mliopata nafasi ya
kuitembelea makumbusho hii mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na
dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania”