Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Sep 12, 2016

Msichana mbaroni kwa kutoa mimba

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia msichana, Elizabeth Benjamini (20) anayedaiwa kutoa mimba ya miezi minane na kisha kufukia mwili wa mtoto. Viungo vya mwili wa mtoto huyo vilizagaa hovyo mitaani huku mbwa wakifanya kitoweo.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Elias Mwita amethibitisha leo kukamatwa kwa msichana huyo Septemba 9, mwaka huu.
Alidakwa baada ya jeshi hilo kupata taarifa kutoka kwa raia wema. Askari walimkamata nyumbani kwake mtaa wa Butengwa, Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Mwita amesema katika mahojiano, msichana huyo alikiri kufanya kitendo hicho na kueleza kuwa katika maelezo ya awali, msichana huyo alieleza kuwa yeye ni mfanyakazi wa baa iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Alisema bado wanaendelea na mahojiano na baada ya kukamilika, watamfikisha mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.
Wakazi wa mtaa huo, Tuma Masanja na Monicka Hassan, walipozungumza na mwandishi wa habari hizi jana, walisema kuwa baada ya tukio kutokea hawakufahamu aliyehusika na unyama huo.
Lakini, baada ya siku moja kupita walishangaa kuona askari wakifika kwenye nyumba anayoishi msichana huo, aliyefika hapo kumtembelea dada yake, ambapo katika mahojiano alikiri kutoa mimba ya miezi sita na kufukia mtoto nje kidogo ya nyumba hiyo.
“Sisi tulishangaa kuona msichana huyo anaongoza moja kwa moja akiwa ameambatana na askari eneo ambalo anadai ndio alizika kiumbe hicho, wakajiridhisha na kumuona hali yake ilivyo kisha wakaondoka naye kwenda kituoni, lakini dada yake alikuwa akikataa kuwa ndugu yake si mhusika wa tukio hilo,” amesema Monica.
Mwenyekiti wa Mtaa huo, Juma Derefa alisema kuwa msichana aliyetupa mtoto na viungo vyake kuzagaa hovyo mitaani, amepatikana na tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi, ambapo lilibaini kuwa alikuwa ni mjamzito.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP