Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Sep 20, 2016

Nguli wa muziki Afrika Kusini Mandoza afariki dunia

Nguli wa muziki nchini Afrika Kusini, Mduduzi Tshabalala, al-maarufu Mandoza, amefariki baada ya kuugua saratani kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 38.
Mandoza alisifika kwa albamu kadha za muziki aina ya Kwaito, aina ya muziki wa Afrika Kusini ambao hukaribiana sana na Hip Hop.

MandozaImage copyrightYOUTUBE

Nyimbo zake nyingi sana zilivuma, zikiwemo nyimbo kutoka albamu yake ya kwanza Nkalkatha. Familia ya Mandoza imesema mwanamuziki huyo aligunduliwa kuwa na saratani baada ya kuanza kuumwa na kichwa sana pamoja na kutatizwa na macho mwaka mmoja uliopita.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP