Nchini Tanzania katika mkoa wa Arusha wilayani Monduli, mzee mwenye zaidi ya miaka 100 ana watoto zaidi ya 70 na wajukuu 300.
Mzee Meshuko Ole Mapi, almaarufu Mzee Laibon, amelazimika kuwa na shule yake na soko kwa ajili ya jamii yake hiyo na anasema bado ana azma ya kuendelea kuoa,Watu kutoka mataifa mbali mbali hufika kumtembelea mzee huyo kama sehemu ya utalii.
Na mwandishi wa BBC Esther Namuhisa alimtembelea mzee huyo Kaskazini mwa Tanzania.


Soko la mzee laiboni ambalo huvutia watalii
Image captionSoko la mzee laiboni ambalo huvutia watalii

Aliwasili katika himaya ya mzee Laiboni na kuona soko linalouza vitu vya asili ambapo aliwaona kina mama na vile vile watoto wengi tu,na kufanikiwa kuzungumza na baadhi ya wanawake hao.
Mwanamke mmoja anayeuza vitu vya watalii kama bangili na shanga, alimwelezea kwamba soko hilo linaundwa na wanafamilia wa mzee Laibon,na si la kawaida kama yalivyo masoko mengine,kwa sababu bidhaa zinazouzwa hapo,wateja wake huwa watalii wanaoshangazwa na maajabu ya mzee Laiboni kuwa na watoto 70 na wajukuu 300,licha na kuwa na wake wachache.
Katika eneo hilo mwandishi huyo aliona nyumba zaidi ya arobaini hivi,na chini ya mti mmoja akakutana na mzee Laiboni ambaye amepumzika


Nyumba takriban 40 za mzee laiboni
Image captionNyumba takriban 40 za mzee laiboni

Alimuuliza idadi ya familia yake na shule aliyoanzisha na kwa sababu mzee huyo hajui lugha ya kiswahili alikuwa na mkalimani wake ambaye alimtafsiria lugha ya kiswahili
Mkalimani wake alisema kuwa mzee Laiboni ana wake wanane na takriban watoto sabini na sita mbali na wajukuu karibu mia tatu.
Kuhusu ni vipi angeweza kuhudumia familia yote hiyo licha ya umri wake alisema kwamba,wakati wa kiangazi yeye huuza ngombe na kununua mahindi


Familia ya mzee laiboni ndio inayoendesha biashara katika soko
Image captionFamilia ya mzee laiboni ndio inayoendesha biashara katika soko

Aliongezea kuwa idadi ya ngombe alionao inakaribia 3000.
Mzee laiboni alisema kuwa wazo la ujenzi wa shule,lilijiri kwa sababu watoto wake walikua wanasoma shule ya mbali na kuna wakati walikua wakishindwa kwenda shule kutokana na tembo ambao pia waliwahi kuua mtu.
Baadaye mwandishi huyo alizuru shule ya mzee Laiboni ambapo alikutana na mwalimu mkuu wa shule hiyo.


Shule ya mzee laiboni ambapo asilimia 90 ya wanafunzi ni watoto wake
Image captionShule ya mzee laiboni ambapo asilimia 90 ya wanafunzi ni watoto wake

Mwalimu huyo alisema kuwa licha ya kuwa mzee Laiboni sio mbaguzi ijapokuwa asilimia 90 ya wanafunzi wote ni watoto wake.