Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amesema kuwa polisi wanafuatilia watu karibu elfu kumi na tano nchini Ufaransa wanaotuhumiwa kuwa na msimamo mkali.
Valls amewaambia waandishi wa habari kuwa mashambulio kadhaa ya waislamu yamezuiliwa ,amesema mashambulio mawili yalizuiliwa wiki iliyopita.

Waziri mkuu wa Ufaransa Manual Valls
Image captionWaziri mkuu wa Ufaransa Manual Valls

Polisi walimkamata kijana mmoja nyumbani kwao Paris siku ya jumamosi kwa tuhuma za kupanga shambulio la kisu.