Katika mahakama The Hague, Somalia imejibu shutuma kutoka Kenya katika mzozo wa ardhi, shirika la habari la AFP linaripoti.
Mataifa hayo mawili yamekuwa yakikabiliana kisheria katika mahakama ya kimataifa ya haki (ICJ) kuhusu eneo uliopo mpaka wa baharini baina ya nchi hizo mbili.

Somalia inasema Kenya inarefusha pasi sababu mzozo huo wa umiliki wa bahari inayoaminika kuwa na utajiri wa mafuta na gesi, AFP inaripoti.
Jumatatu, Kenya imetaja tuhuma za Somalia kuwa inataka kuiba akiba ya mafuta na gesi katika eneo hilo, kama ''tuhuma za kutia uchungu na zisizo za kweli".
Somalia inasema imewasilisha kesi hiyo katika mahakama ya ICJ baada ya kujaribu na kushindwa kujadiliana na Kenya.