Ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema kuwa, uchafuzi wa hewa unaigharimu zaidi ya dola trilioni tano kwa mwaka jambo linaloathiri maendeleo ya nchi maskini. Takwimu zimeonyesha kuongezeka kwa ustawi wa matumizi na kupoteza kipato jambo linalochangia kuongezeka kwa vifo vya mapema vinavyotokana na uchafuzi wa hewa.

Ripoti hiyo imeonesha kuwa kifo kimoja kati ya kumi kimesababishwa na hewa chafu, huku vifo vingi vikisababishwa na moshi.China ndiyo imeathirika zaidi, kwa kupoteza karibu asilimia kumi ya pato lake la taifa ikifuatiwa na India and Cambodia znazopoteza karibu asilimia nane kwa sababu ya uchafuzi wa hewa.
Utafiti huo pia umeangazia takwimu za kuanzia mwaka 2013 na miaka ya hivi karibuni ambapo takwimu hizo zinapatikana.