Ndugu Ally Mlangi mkazi wa Mol Ubelgiji leo mchana ametimiza moja ya sunna muhimu ya dini yake baada ya kupiga goti na kukabidhiwa rasmi mke halali bi Nasra.Ndoa ilifungwa jijini Dar es Salaam sehemu za Buguruni.

Mr Ally akimsomea dua maalumu mkewe Mrs Nasra Ally muda mfupi baada ya ndoa kufungwa.

Bi harusi Mrs Nasra Ally akimnyeshwa maziwa mumewe muda mfupi tu mara ya baada ya kuhalalishiwa ndoa yao mchana wa leo jijini Dar es Salaam.

Mr na Mrs Ally wakiwa na nyuso za furaha huku wakiendelea kupata picha za kumbukumbu na ndugu na jamaa zao,pembeni mwa bwana harusi aliyevalia kanzu ni kaka wa bwana harusi ndugu Rashid.
Maganga One Blog inachukua fursa fupi kumpongeza sanaa bwana Ally na mkewe kwa kupiga hatua kubwa muhimu maishani..Mungu awajaalie ndoa yao idumu wazikane na awajaalie kizazi bora inshallah.Hongereni sana tena sana.