Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L.
Kayombo (Kushoto) akiwa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt Mariam Malliwadh mara baada ya kuwasili katika kampuni ya New Habari Corparation




 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L.
Kayombo akisikiliza kelele hizo ambazo zimekuwa zikiwasumbua wafanyakazi wa kampuni hiyo


Kelele ziosizo za kawaida huenda zikawasababishia wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari Corparation matatizo ya kutesikia kutokana na kutokuwa na vifaa madhubuti vya kuzuia kelele hizo.



Hayo yamebainika wakati wa Ziara
ya ghafla iliyofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L.
Kayombo ambapo miongoni mwa mambo yaliyobainika ni pamoja na kelele
hizo zisizo za kawaida ambazo zinazotolewa na mtambo wa kutengeneza magazeti katika
kampuni hiyo ambazo zinahatarisha uwezo wa
wafanyakazi
wa kusikia .




Ziara ya Mkurugenzi Kayombo ya kutembelea katika kampuni hiyo imekukuja muda mfupi baada ya kusikia vilio vya wananchi na wafanyabiashara wanaoishi jirani na kiwanda hicho.



Baadhi ya wananchi wanaofanya biashara jirani na eneo hilo wamesema kuwa kwa muda mrefu
wametoa malalamiko yao lakini hayakufanyiwa kazi, hivyo kuamua kufikisha kwa
kiongozi shupavu mwenye nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi Mh. John
Kayombo.




Baada ya
malalamiko ya wananchi kumfikia ,bila kupepesa macho Mkurugenzi Kayombo
akaenda New Habari House bila kutoa taarifa kwa uongozi wa kiwanda kwa
nia ya kuona hali halisi.




Akiwa kiwandani hapo Mkurugenzi
Kayombo alikagua maeneo mbalimbali yanayozunguka kiwanda na hatimaye
akafika kwenye mashine inayochapisha magazeti yanayotolewa na kampuni
hiyo.




Mashine hiyo ilikuwa inapiga kelele hali ambayo sio rahisi
kwa binadamu kukaa eneo hilo lakini alikuta wafanyakazi wakiwa hapo
tena bila kifaa chochote cha kuzuia au kupunguza sauti hizo.





'' Hili jambo sio zuri haiwezekani mashine ipige kelele kiasi hiki
huku wafanyakazi wakiendelea kuzalisha magazeti,huu ni ukatili na ni
kwenda kinyume na haki za binadamu"alisema Kayombo.