Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Oct 20, 2016

Mapigano kusitishwa kwa siku tatu Yemen

Mpango wa kusitisha mapigano kwa siku tatu unakaribia kuanza nchini Yemen.
Upande wa serikali ambao unaungwa mkono na Saudi Arabia na waasi wa Houth wamekubaliana na umoja wa mataifa kusitisha mapigano.
Kunaripoti zisemazo kuwa mapigano makali yanaendelea mpaka kufikia kusitisha mapigano, na kuna tetesi kwamba yatasitishwa.
Lakini umoja wa mataifa unatumaini kuwa kusitisha mapigano kunaweza kupelekea kuendelea kwa mazungumzo ya amani.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, takriban watu 7,000 wameuawa katika mapigano hayo
Image captionKwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, takriban watu 7,000 wameuawa katika mapigano hayo

Kwa zaidi ya miezi minane ya vita ya wenyewe kwa wenyewe kumeleta hali ngumu ya maisha kwa raia nchini Yemen.
Kwa sasa zaidi ya watoto milioni moja wanabiliwa na utapiamlo kwa kiwango cha juu.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP