Marekani imeelezea kusikitishwa kwake kuhusu ripoti kutoka Iran inayosema kuwa Wairani wawili wenye asili ya Marekani wamehukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani.
Msemaji wa idara ya nchi hiyo Mark toner ametaka kuachiliwa mara moja kwa mfanya biashara, Siamak Namazi na baba yake Baquer, ambaye aliwahi kuwa muwakilishi wa UNICEF na gavana wa Iran.
Shirika la habari la serikali nchini Iran linasema kuwa wamehukumiwa kwa kosa la kushirikiana na serikali hasimu ya Marekani.
Siamak Namazi alikamatwa mwaka mmoja uliopita alipoitembelea Tehran.
Baba yake alikamatwa mwezi Februari katika safari ya kujaribu kumuokoa mwanawe ili kuachiliwa huru.
0 Comments