Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani), kwa siku tatu mfululizo hadi jana jumapili Oktoba 16, 2016 alihudumu katika Kilele cha Mkutano Mkubwa wa Injili uliofanyika Kanisa la EAGT Posta B, Mabatini Jijini Mwanza, uliofanyika kwa juma zima kuanzia Oktoba 09 hadi Oktoba 16 mwaka huu.
Ulikuwa Mkutano uliojaa Neema ya Mungu ambapo makumi kwa mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza, walimgeukia Kristo na kuokoka huku waimbaji mbalimbali ikiwemo Kwaya ya Havillah, Mwanyamaka, Emmanuel Mgogo, Elineema Babu pamoja na waimbaji wengine wengi wakihudumu katika mkutano huo.
Mchungaji Kulola aliwahimiza wakristo kuweka dini zao pembeni na kumtumikia Mungu kwa roho na kweli huku wakiacha tabia ya kumuonea Kristo aibu.
"Tujivunie maamuzi tuliyonayo ya kuokoka maana hatukufanya makosa na kwa kuwa tunaye Yesu Kristo ambaye neno lake linakatakata kama upanga naomba wote tuwe vichaa kwa ajili yake". Alisisitiza Mchungaji Kulola akiwataka waliokoka kumtumikia Mungu bila hofu yoyote.
Na BMG
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiendelea kunena neno la Mungu katika mkutano huo
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiendelea kunena neno la Mungu katika mkutano huo
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiendelea kunena neno la Mungu
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Posta B, Mabatini Jijini Mwanza, Lameck Nkumba, akiomba kwenye Mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo Mchungaji wa Kanisa la EAGT Posta B, Mabatini Jijini Mwanza, Lameck Nkumba (kulia).
Waumini wakifuatilia mkutano huo
Baadhi ya waumini wakifuatilia mkutano huo
Waumini wakifuatilia mkutano huo
Bonyeza HAPA Kuhusu Mkutano Huo.
0 Comments