Maafisa katika mji wa kusini mwa Somalia wa Baradhere wamewataka wake wa wapiganaji wa al-Shabab kuondoka katika kipindi cha juma moja.
Mkuu wa wilaya hiyo amewashutumu wake hao kwa kuwapelelezea waume zao ,akiongezea kuwa watakamatwa iwapo hawataondoka.
Amesema kuwa operesheni ya kijeshi ya kuwafurusha katika sehemu hiyo itafanyika hivi karibuni .
Kundi la wapiganaji wa al-Shabab lilipoteza udhibiti wake wa mji huo mwaka uliopita lakini linaendelea kuushambulia mara kwa mara.
|
0 Comments