Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akihojiwa na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, kuhusiana na sakata la Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza kugoma kukabidhi mihuri yao ya utendaji kazi.


Na George Binagi-GB Pazzo
"Hii mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ni dili, hivyo haitambuliki kwa sasa, kwanza imesababisha migogoro mingi kwa wananchi ikiwemo uuzaji wa viwanja kiholela". Amesisitiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba.



Ameshikilia msimamo wake kwamba mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza haitambuliki kama awali alivyosema kwamba waikabidhi ofisini kwake.

Leo Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza wameendelea kushikilia msimamo wao wa kutorudisha mihuri hiyo huku wakitishia kutoshirikiana na Watendaji Jijini Mwanza.

Juzi jumamosi Wenyeviti 174 wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza, walivunja kikao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, baada ya Mkurugenzi huyo kuwataka kukabidhi mihuri yao. 
#Lakefm #BinagiBlog #BMG #Mwanza