Washambuliaji wenye silaha wameshambulia kituo kimoja cha mafunzo ya upolisi katika mji wa Quetta huko Pakistan
washambuliaji sita waliingia katika mabweni ya wanafunzi wa kituo hiko na kuwashambulia, mamlaka zinasema kuwa watu takribani 50 wameuawa wakiwemo wanafunzi wa kituo hiko na walinzi. huku wengine wakijeruhiwa.
Majeruhi walepelekwa katika hospitali za ndani.
Mamia ya wanafunzi waliokolewa kutoka Chuo cha polisi cha Balochistan wakti wanajeshi walipowasili kupambana na washambuliaji hao.
washambuliaji wanne wameripotiwa kuuwawa katika makabiliano na jeshi pamoja na polisi, hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na shambulio hilo.
Waziri wa mambo ya ndani Mir Sarfaraz Ahmed Bugti amesema kuwa idadi ya waliopoteza maisha katika shambulio hilo inaweza kuongezeka.
Sauti za milio ya milipuko na risasi zilikua zikisika vizuri, alisema shuhuda mmoja wa tukio hilo.
"walikua wakikimbilia katika majengo yetu huku wakifyatua risasi, sisi tulikimbilia juu na baadae kuruka chini ili kuokoa maisha yetu'' mkufunzo wa kituo hiko aliimbia televisheni ya Geo.
Quetta ni jimbo kuu la mji wa Balochistan, ambao umeshawahi kupata mashambulizi kutoka kwa makundi yanayojitenga pamoja na wanajeshi wa kiislamu.
Mwezi nane watu 88 waliuawa katika mashambulio tofauti ya mobamu yaliyolenga hospitali na wanasheria huko Quetta.
0 Comments