Pichani
Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana
kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili
kuwaka moto .

Basi
lenye namba za usajili T990 AQF la kampuni ya Safari Njema liililokuwa
likitokea Dodoma kuja jijini Dar, limeteketea kwa Moto maeneo ya Kimara
Stop Over-Suka,mara baada ya kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake
za usajili hazikujulikana mara moja),jioni ya leo,Inaelezwa kuwa mali zote zilikowemo katika
basi vimeteketea kabisa kwa moto,hali ya abiria waliokuwemo ndani ya
basi hilo tutawaleta taarifa kamili itakayotolewa na Jeshi la Polisi.

Baadhi ya Wakazi wa eneo la Kimara Stop Over na Kimara Suka wakielekea kushuhudia eneo la ajali kati ya basi la Safari Njema na Lori lililokuwa limebeba shehena kubwa ya mifuko ya Cement.