|
RAIS John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi Dar es Salaam jana, ilisema Rais ametengua uteuzi huo kuanzia jana Oktoba 29, mwaka huu na atapangiwa kazi nyingine.
Kijazi alisema kufuatia uamuzi huo, uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa Makosa ya Jinai utatangazwa hapo baadaye.
Athumani aliteuliwa kushika nafasi hiyo mwezi Mei mwaka jana na Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.
Kabla ya uteuzi huo, Athuman alikuwa Kaimu Kamishna wa Kamisheni ya Intelijensia ya Jinai.
Alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Robert Manumba, ambaye alistaafu kwa mujibu wa Sheria.
Athuman amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi, ikiwemo Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Mbeya
0 Comments