Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Oct 12, 2016

Putin afuta ziara nchini Ufaransa

Rais wa Urusi Vladimir Putin amefuta ziara yake nchini Ufaransa wakati unaendelea kushuhudiwa mzozo kuhusu Syria.
Alitarajiwa kukutana na Rais wa Ufaransa Francois Hollande na kufungua kaniss jipya la Orthodox baadaye mwezi huu.
Lakini baada ya serikali ya Ufaransa kusema kuwa mazungumzo yataegemea zaidi suala la Syria ziara hiyo ilifutwa.

Ufaransa ina wasi wasi na mashumbulio yanayoungwa mkono na Urusi mjini AleppoImage copyrightAFP
Image captionUfaransa ina wasi wasi na mashumbulio yanayoungwa mkono na Urusi mjini Aleppo

Siku ya Jumatatu Hollande alipendekeza kwamba Urusi inafaa kushtakiwa kwa uhalifu wa kivita kutokana na mashambulio ya mabomu yanayotekelezwa na ndege za kivita za Urusi mjini Aleppo, Syria.
Bwana Hollande aliiambia runinga moja ya Ufaransa kwamba taifa hilo linafaa kushtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Alidokeza pia kwamba huenda angekataa kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin, wakati wa ziara hiyo
"Hawa ni watu ambao ni waathiriwa wa uhalifu wa kivita. Wanaotenda haya wanafaa kuwajibishwa, hata kama ni katika mahakama ya ICC," Bw Hollande aliambia TMC.

Urusi imekanusha madai kwamba inashambulia raia na badala yake imekuwa ikisisitiza kwamba inawashambulia magaidi.
Image captionUrusi imekanusha madai kwamba inashambulia raia na badala yake imekuwa ikisisitiza kwamba inawashambulia magaidi.

Wiki iliyopita, Urusi ilitumia kura ya turufu kupinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa urushaji mabomu Aleppo.
Azimio hilo lilikuwa limewasilishwa na Ufaransa na Uhispania.
Urusi imekanusha madai kwamba inashambulia raia na badala yake imekuwa ikisisitiza kwamba inawashambulia magaidi.
Urusi na Syria si wanachama wa ICC.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP