Raia nchini Ivory Coast wanahusika leo katika shughuli za upigaji kura ya maoni, kuhusiana na upatikanaji wa katiba mpya ya nchi hiyo -- ambapo Rais Alassane Ouattara, anasema kwamba italisaidia taifa hilo kusonga mbele baada ya miaka mingi ya ghasia.
Vyama vya upinzani vimetoa wito wa kususiwa kwa shughuli hizo, vikisema kuwa rasimu hiyo ya katiba inafanywa kwa haraka ili kumpa nguvu zaidi Rais Ouattara.
Kipengee kimoja katika mapendekezo ya rasimu hiyo ya katiba mpya, inalegeza kamba kuhusiana na uraia wa mgombea kiti cha Urais-- swala ambalo limechochea mapigano ya mara kwa mara nchini Ivory Coast tangu mwaka 2002.
Pia, inabuni bunge la senati -- ambalo robo tatu ya wabunge watakuwa wakiteuliwa moja kwa moja na Rais
|
0 Comments