Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 12, 2016

Ali Kiba Awatolea ‘Povu’ Wanaomtukana Wizkid Mitandaoni Kuhusu MTV EMA

DAR ES SALAAM: IKIWA ni baada ya waandaaji waTuzo za MTV EMA 2016 kumpokonya tuzo ya Best African Act mwanamuziki wa Nigeria, Wizkid na kuahidi kumkabidhi Mbongo Fleva, Ali Kiba, kumekuwa na minonong’o mingi na comment mbaya za mashabiki mitandaoni wakimshambulia kwa matusi na kejeli Wizkid aliyepewa tuzo hiyo kimakosa.

Hali hiyo imemfanya Alikiba afunguke na kuelezea namna anavyokerwa na baadhi ya watu wanavyomshambulia Wizkid ilihali wao Kiba na staa huyo wote ni wanamuziki na hawajawahi kugombana.
Kiba hakukomea hapo, alienda mbali zaidi kwa kupost picha ya aliyopiga akiwa na Wizkid na kuandika maneno haya kwenye akaunti yake ya Instagram.
“Sijafurahishwa na ninachokiona kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii, ninamkubali sana wizkid kama msanii mwenzangu na kama mshabiki pia. Nimesikitishwa sana na kushtushwa kuona watu wakimdhihaki Wizkid kwa maneno yasiofaa na matusi, nataka kuwa muwazi tu naamini kuwa haya maneno yakijinga na yasiyofaa hayahusishi na hayajatoka kwa mashabiki wangu wa kweli kwasababu nafahamu wamekuwa wakijua jinsi gani namkubali Wizkid.
usizamishwe na maneno ya mahater bro, hongera sana kwa kuwa mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwako, upendo wa dhati kutoka kwa mashabiki wangu wa kweli na nchi ya Tanzania pamoja#KingKiba,”Ameandika Kiba.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP