Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 12, 2016

Giggy Money: Mara Nyingi Nashinda Na Nguo Za Ndani (Mpaka Home)

Leo safu hii imetua maeneo ya Kawe jijini Dar, ambapo tumeweza kuyafunua maisha halisi ya mwanadada machachari ambaye sasa hivi yupo ndani ya mjengo wa Radio Choice FM kama mtangazaji, si mwingine ni Gifty Stanford ‘Gigy Money’ ana vitu vingi sana nje ya fani yake ya utangazaji na usanii wa Bongo Fleva, twende pamoja:

Vipi ni msichana wa kutulia nyumbani?
“Najua watu wengi wananichukulia ndivyo sivyo lakini ni hivi, naweza kukaa nyumbani nikapika, nikafanya vitu vyote ambavyo mwanamke aliyeolewa anapaswa kuvifanya, pia sipendi  kutoka pasipo sababu za msingi.
Ni kitu gani kinampa utulivu akiwa nyumbani?
“Napenda kupumzika kutokana na pilikapilika za hapa na pale, kitanda changu kinanipa utulivu wa nafsi yangu kama nikichoka na nikitaka kuwaza mambo mengine hapo ndipo mahali pangu.
Vipi kuhusu usafi wa nyumbani kwake?
“Napenda sana nyumba mimi na kila wakati nilikuwa nawaza kuwa na nyumba yangu kabisa kwani napenda maua ili ya-pende-zeshe nyumba yangu lakini ukiwa na za kupanga kama hii ninayoishi, huwezi kujiachia hivyo.
Mambo ya jikoni Veepe?
“Kwa upande wa jikoni niko vizuri kabisa ndiyo maana umekuta jiko, vyombo na vitu vyote ila nikipiga vitu vyangu kichwani (pombe) mambo ya chakula siyo mahali pake kabisa.
Anaishi na nani?
“Hapa mara nyingi naku-waga na mpenzi wangu Mo (mta-ngazaji pia), japokuwa siishi naye moja kwa moja lakini ndiye mtu wangu, mara nyingi tupo pamoja sana.
Anaishije na majirani?
“Naishi na majirani zangu vizuri sana hata siku ukinikuta huwezi amini kama ndiyo mimi kwa sababu niko nao vizuri sana  wala sina hata chembe ya madhara.
Anapendelea mavazi gani nyumbani?
“Vazi langu la nyumbani ni chupi na sidiria au shati ndiyo najisikia raha kama niko nyumbani na si kitu kingine chochote.
Anapenda kupika chakula gani?
“Napenda sana ndizi kwani ni chakula ambacho naweza kukipika sana na hata nile wiki nzima sikichoki.
Ni mwanamke
wa aina gani?
“Najua watu wengi wanavyoniona kwenye mitandao wananichulia hivyo kwamba mapepe lakini ni tofauti kabisa na maisha yangu ya kila siku ninavyoishi, mimi ni mwanamke tena zaidi ya wanawake wanaosifika kwenye macho ya jamii ndiyo maana mpenzi wangu alivyonijua vizuri ananipenda na kuniheshimu.”

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP