Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akiwa na Msimamizi wake, Joe Anena (kulia) muda mfupi kabla ya kukwea pipa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Kuelekea mjini Huxleys, Kreuzberg, Berlin kunako mpambano wa marudio kati yake na Bondia Zapir Rasulov, baada ya lile la kwanza kushinda kwa point kule nchini Panama City, Panama na kurudi na ubingwa.