Na George Binagi-GB Pazzo

Baadhi ya Wafanyabiashara ndogondogo kwenye Masoko na Minada katika Halmashauri za Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza, wamelalamikia uchafu kukithiri katika maeneo yao ya kufanyia biashara hali ambayo inawasababishia kero bubwa.





Wakizungumza na Lake Fm, wafanyabiashara hao wamesema hali hiyo inawapa kero kubwa ikiwemo harumbu mabya, licha ya kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kipindupindu.



Katika masoko na minada mbalimbali ikiwemo Kitangiri, mrundikano wa uchafu katika maeneo ya kukusanyia uchafu imeelezwa kuwa kero kubwa hadi kwa makazi jirani huku changamoto ya ukosefu wa vyoo ikiibua malalamiko zaidi.



Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara ndogondogo kwenye Masoko na Minada mkoani Mwanza, Justine Sagara, alisema changamoto hiyo imesababishwa na halmashauri za Ilemela na Jiji la Mwanza kushindwa kuondoa uchafu kwa wakati hatua ambayo imepelekea baadhi ya machinga kugoma kulipa ushuru kwa ajili ya usafi.



"Tuliomba watujengee vyoo lakini ombi letu bado halijafanyiwa kazi ambapo hadi sasa ni Soko la Kiloleli tu ndo lenye choo, lakini masoko na minada mingine hakuna vyoo". Anabainisha Sagara.