Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 19, 2016

Magufuli ateua wenyeviti PSPF, LAPF

RAIS John Magufuli, amefanya uteuzi wa wenyeviti wawili wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii na mmoja wa chuo.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi Dar es Salaam imewataja walioteuliwa kuwa ni Alhaji Mussa Iyombe aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Mhandisi Iyombe ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Rais Magufuli pia amemteua Profesa Faustine Karani Bee kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF).
Profesa Karani Bee ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemteua Profesa Tadeo Andrew Satta kuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Kabla ya uteuzi huu Profesa Satta alikuwa akikaimu nafasi hiyo.


Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP