Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 11, 2016

Mama atukanwa kwa kumnyonyesha mwanawe mkahawani

Mama mmoja amezungumza baada ya kutukanwa kwa kumnyonyesha mwanawe ndani ya mkahawa mmoja huko Belfast.
Liz Skelcher alikuwa akimnyonyesha manawe wa wiki 11 Evie katika mkahawa wa Nandos wakati kisa hicho kilipotokea wiki iliopita.
Mkahawa huo umesema kuwa unaruhusu akina mama kunyonyesha wana wao
Lakini ilikuwa wateja wengine wa kike waliomtusi mwanamke huyo aliyekitaja kisa hicho kama cha kutisha na kushangaza.
Akizungumza na kpindi cha BBC cha Talkback, bi. Skelcher alisema: Nilikuwa katika mkahawa huo na mumewangu pamoja na mamake mume wangu wakati Evie alipoamka na akataka kunyonya,nilimuinua na kumuweka katika titi moja.

Mkahawa wa Nandos ambapo mama huyo alitukanwa kwa kumyonyesha mwanawe
Image captionMkahawa wa Nandos ambapo mama huyo alitukanwa kwa kumyonyesha mwanawe

Kulikuwa na wanawake watatu katika meza moja na mmoja wao hakupendelea mimi kumnyonyesha mwanangu.
Aliniambia kwamba tulikuwa tunamkera kumyonyesha mtoto katika mkahawa.
Aliendelea kunitusi mbele ya marafikize na alipoulizwa shida yake ilikuwa nini,alisema hakutaka kuona matiti yangu wakati alipokuwa akila chakula chake cha jioni

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP