Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 11, 2016

Zuma aepuka kura ya kutokuwa na imani naye

Kura ya kutokuwa na imani dhidi ya rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma imeshindwa kufaulu katika bunge licha ya madai ya hivi karibuni ya ufisadi.
Uchunguzi wa tume ya kukabiliana na ufisadi nchini humo wiki iliopita ulizua madai ya utovu wa nidhamu dhidi ya rais Zuma.

Chama cha cha rais Zuma ANC kina wabunge wengi katika bunge na mswada huo wa upinzani ulishindwa kwa kura 214 dhidi ya 126.
Hii ni kura ya tatu ya kutokuwa na imani naye iliowasilishwa bungeni katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja.
Uchunguzi uliofanywa na tume ya kukabiliana na ufisadi nchini humo ulisema kuwa jopo la majaji linafaa kubuniwa ili kuchunguza madai ya uhalifu katika serikali ya Zuma.
Uchunguzi huo ulipata ushahidi kwamba familia ya Gupta ilio na uhusiano mkubwa na rais Zuma huenda ilikuwa na ushawishi mkubwa katika uteuzi wa baraza la mawaziri.
Zuma na familia hiyo wamekana kufanya makosa yoyote.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP