Taarifa kutoka vyombo vya serikali huko mjini Washington zimeeleza kuwa Marekani imetoa kibali kwa kampuni ya ndege ya Airbus kuuza ndege mia moja Nchini Iran.
Kampuni ya kutengeneza ndege ya Ufaransa imethibitisha kupokea leseni ya pili kutoka Marekani ikiazimia kuuza ndege nchini Irani.

Kampuni hiyo ya ndege ya Airbus inalazimika kupata leseni hiyo ili kuboresha biashara na nchi ya Iran ukizingatia kwamba asilimia kumi ya vifaa vya ndege hizo hutengenezwa nchini marekani.
Suala la kuuzwa kwa ndege hizo nchini Iran limetokana na makubaliano ya mpango wa kinyuklia wa Tehran, ingawa leseni hiyo huenda ikasitishwa katika uongozi mpya wa Rais mteule wa Marekani Donald Trump.