Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amepongezwa
na walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Matosa iliyopo Kata
ya Goba , Manispaa ya Ubungo kwa kufanikisha kwa kiasi kikubwa
utekelezaji wa mradi wa SEDP II.



Mradi huo unaohusisha ujenzi wa vyumba viwili vya darasa, nyumba za
walimu, kisima cha maji, tanki la kuhifadhia maji pamoja na vyoo upo
katika hatua nzuri ya kukamailika kutokana na juhudi pamoja na utendaji
kazi uliotukuka wa Mkurugenzi Kayombo akishirikiana na watumishi wa
Manispaa hiyo.


Akizungumza na mtandao wetu mwalimu Mkuu wa shule
hiyo alisema amefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Mkurugenzi wa
Manispaa hiyo za kuleta maendeleo kwa wananchi na kwenda sambamba na
kauli mbiu ya Rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu.


"Napenda
kutoa shukrani Kwa Serikali kwa kuuleta mradi wa SEDP II katika shule
yetu, pia napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo kwa juhudi zake anazozifanya mpaka mradi
umefika hatua hii, kwa kweli ametusaidia sana, mungu ambariki", alisema
Mwalimu mkuu.




Wakati huo huo wanafunzi wanaosoma katika shule
hiyo wamempongeza Mkurugenzi Kayombo kwa kazi nzuri aliyofanya mpaka
kuweza kufanikisha kupatikana kwa maji pamoja na madarasa, vyoo, tanki
la maji na nyumba za walimu.