Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 30, 2016

MOBISOL NA ZUKU TV WAZINDUA HUDUMA ZA TELEVISHENI YA SATELITE YA NISHATI YA JUA Meneja Mkuu wa Zuku
Tv Tanzania  , Bw.Omari Zuberi akiongea na waandishi
wa habari juu ya huduma mpya ya
TV ya nishati ya jua ambayo ina
channel za
Zuku Tv
 katikati ni Afisa masoko wa Mobisol
Sjors Martens akiwa na wafanyakazi wa mobiso l katika uzinduzi huo hii
leo jijini Arusha

 Mmoja wa mmteja wa mobisol ambaye akutaka kutaja jina lake akiongea wakati wa uzinduzia ambapo
aliisifia kampuni ya mobisol nakusema ni mtetezi wa wananchi wanaoishi
vijijini ambapo umeme haujafika
 Meneja wa zuku Tanzania wa
kwanza kushoto akibadilishana mawazo na wa kwanza kulia ni afisa
usiano wa Zuku  dada Yasta pamoja na  mwakilishi wa
zuku  Jack Karanja katika uzinduzi
 wafanyakazi wa zuku wakifurahia
mara baada ya uzinduzi


 Na Woinde
Shizza,Arusha

 KAMPUNI
inayoongoza kwa utowaji wa huduma za
nishati ya jua majumbani ,Mobisol na Kampuni ya Zuku Tv inayotoa burudani za
satellite wameungana  pamoja kwa ajili
kuwanufaisha watanzania wasiounganishwa na nishati ya
umeme. 

Kwa pamoja kampuni
hizi zimezindua kwa mara ya kwanza TV ya nishati ya jua ambayo ina channel za
Zuku Tv  huduma inayowalenga wale ambao
hawajafikiwa na umeme wa gridi ya Taifa.Huduma hii huunganisha
mfumo  wa nishati jua, televisheni ya hadi inchi 32
ya nishati jua, ungo wa satellite, na huduma ya ya kifurushi cha Zuku Smart
Plus chenye chanelli 47 and 18 za redio. Mobisol wanalenga
kutoa huduma hii kwa watanzania ambao hawajafikiwa
na huduma ya nishati ya umeme, kwa  kutoa
nashati safi na ya kuaminika kwa bei nafuu popote ulipo katika mfumo moja
mkamilifu.Mobisol inatoa vifurushi
mbalimbali vya nishati ya jua ya
majumbani, vilivyo na uwezo wa kutoa nguvu ya umeme hadi
200W,  unaotosha matumizi ya kaya nzima. Kila
kifurushi kintaota paneli ya PV, betri ya nishati ya jua, taa nne za mwanga
mkali,TV kubwa ya kioo cha  bapa, tochi,
chagi ya simu na redio ambayo unaweza kuichagi. Vifaa hivi vinapatikana na
waranti, huduma ya kufungiwa bure, huduma ya wateja na huduma ya marekebisho
kwa miaka 3.  Pia,
Kwa kuongezaTsh 8,999 kwamwezikwakifurushi,
watejawatawezakupatahudumazaZuku
TV kwamudawamasaasabakwasiku .Akizungumza katika
uzinduzi  huo   Afisa masoko wa Mobisol
Sjors Martens alisema kuwa wao wanania ya kuleta maisha mazuri kwa wateja
wao nchini Tanzania. 
Alisema Huduma yao  ya
kifurushi cha televisheni ya satellite
kitawezesha wateja  kufurahia habari , michezo, burudani na maudhui ya
elimu wakati wowote hata wakiwa wanaishi
mjini au vijijini.Kwa upande wake Meneja Mkuu
wa Zuku Tv Tanzania  , Bw.Omari Zuberi alisema
ubunifu wa huduma
hii itatuwezesha kufikia zaidi ya watanzania million 8 ambao hawajawa na
nishati ya umeme wa grid ya Taifa na kutuwezesha kuchangia kwa asilimia kubwa
ongezeko la televesheni
nchini. 

  “Hii ni
fursa ya kipekee na ya kuleta hamasa  kwa
wateja wa Mobisol kuwa na uwanja mpana zaidi
wa kuchagua na kufurahia zaidi ya chaneli 40 za Zuku TV inayotambulika
kama huduma bora ya bei nafuu inayotoa burudani kwa
familia kwa kuhamasisha  maudhui ya
kinyumbani zaidi,” alisema Zuberi.Aliongeza kuwa Ingawa
asilimia 70 ya watanzania hawajafikiwa na huduma ya
nishati ya umeme na asilimia kubwa ya watanzania bado hawana Televisheni,
Mobisol na Zuku wametumia fursa hii na kuungana pamoja kwa ajili ya kutoa
huduma ya umeme wa jua na kutoa burudani ya TV Satellite yenye ubora wa
kimataifa Aidha alisema kuwa
Huduma hii ya PayTV  iliozinduliwa mkoani hapa itapatikana katika
mikoa ambayo
Mobisol inatoa huduma ambapo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani,
Singida, Tabora, Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera, Simiyu, Mbeya,
Songwe na Njombe - na baadaye kote nchini mwaka
ujaoAlibainisha kuwa Kupitia Zuku
TV, watanzania wanaweza kufurahia idadi ya
channel  za kusisimua ikiwa ni pamoja na
channel  za nyumbani  FTA,
channel
za kimataifa na channel za  Zuku
asili; Zuku Sports, hivi karibuni ilizindua tena
Zuku Swahili, Zuku Kids, Zuku Life Glam na
Zuku Nolly.Alisema kuwa Bei ya kifurishi
cha Zuku smart pack kitakuwa kikiongezwa
kwa awamu katika mfumo nishati ya
jua  ya Mobisol, ambayo wateja hulipa
kupitia  simu  kwa kipindi cha
miaka mitatu.

Alifafanua kuwa  Baada
ya miaka
mitatu, wateja watamili hivyo vifaa  na
kupata ofa ya kuvutia kwa kulipa tena huduma hiyo
mpya
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP