Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 11, 2016

Obama: 'Ninamuunga mkono' Donald Trump

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ni ''heshima'' kubwa kukutana na rais Barrack Obama katika mazungumzo ya mpito yaliofanyika katika ikulu ya White House.
Bwana Obama amesema kuwa ametiwa moyo kuhusu mazungumzo yao ya maswala mbalimbali yaliochukua zaidi ya saa moja.

Obama na Trump wakisalimianaImage copyrightAFP
Image captionObama na Trump wakisalimiana

Bwana Trump ametilia shaka uraia wa rais Obama na kuapa kuharibu ufanisi wake wakati wa utawala wake.
Wakati wa kampeni bwana Obama alisema kuwa bwana Trump 'hafai' kuongoza Marekani.
Hatahivyo Obama alisema kuwa ''anamuunga'' mkono baada ya kumshinda Hillary Clinton.

Maamkuzi ya kihistoria kti ya Trump na ObamaImage copyrightAFP
Image captionMaamkuzi ya kihistoria kti ya Trump na Obama

Baada ya mkutano huo wa ikulu rais Obama alisema kuwa kipaombele chake sasa katika miezi miwili ijayo ni kuhakikisha kuwa kundi litakalosimamia shughuli za mpito linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa wamezungumza sera za nyumbani pamoja na zile za kigeni na kwamba amefurahishwa na maoni ya Donald Trump kwamba yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika maswala yanayokabili Marekani.
Bwana Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika siku zijazo.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP