Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 28, 2016

RC SINGIDA AANZA ZIARA KUTEMBELEA KATA 136 ZA MKOANI SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara Kijijini Doroto
 Baadhi
ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi
Methew Mtigumwe katika ziara yake katika Halmashauri ya Itigi

Mkuu
wa Wilaya ya Manyoni Mhe Godfrey Mwambe akiongea na wananchi katika
ziara ya mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew J. MtigumweNa Mathias Canal
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii leo
ameanza ziara ya kikazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za
wananchi katika Mkoa wa Singida.
Rc Mtigumwe ameanza ziara yake hiyo katika Halmashauri ya Itigi, iliyopo
katika Wilaya ya Manyoni ambapo atatembelea kata zote za halmashauri
hiyo.Pamoja na kutambua kero za wananchi na mambo mengine pia
Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida anatumia mikutano hiyo maalumu kwa ajili ya
kufahamiana na wanachi ikiwa ni pamoja kusikiliza kero zao ambazo
zimewasua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi.Mtigumwe akiwa
katika Kijiji cha Doroto amehimiza zaidi wananchi kuandaa vyema mashaba
yao na kuzingatia kilimo chenye kustahimili ukame kwani kuna mabadiliko
makubwa ya tabia nchi jambo ambalo limepelekea kuchelewa kuanza kwa
mvua.Mhe Mtigumwe amewaagiza maafisa kilimo wa Kata na Wilaya
zote za Mkoa wa Singida kutokaa ofisini kipindi hiki cha msimu wa kilimo
badala yake kwenda mashambani kuwasaidia wananchi mbinu bora za kilimo
sambamba na kuwasaidia namna bora ua kuandaa mashamba.Sambamba
na hayo pia amewasisitiza wananchi kuzingatia maelekezo watakayopatiwa
na Maafisa kilimo ili kuwa na uhakika wa kuvuna mazao mengi zaidi kwa
kilimo chenye tija.Katika ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Singida
Mhandisi Mathew Mtigumwe ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya
Mkoa wa Singida.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP