Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya awamu ya tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya afya ikiwemo kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa Afya na kuimarisha miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kote nchini.


Amesema hayo wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo katika viwanja vya Green Ground, Oysterbay Jijini Dar es Salaam baada ya kuongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika matembezi ya hisani ya kilomita 4.2 ya kuchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi, wakunga 400 katika ngazi mbalimbali kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning nchini.