Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed akimpa pole Mhe. Mapuri aliyekuwa Hospitali ya Muhimbili akipatiwa matibabu.
Serikali imesikitishwa na taarifa za uvumi na uzushi uliosambazwa jana na leo kwenye mitandao ya kijamii, taarifa hizi siyo za kweli na tunawaomba wananchi wazipuuze.
Aidha, Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa Serikali.
Imetolewa na : Dk. Juma Mohammed Salum Kny Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Zanzibar
|
0 Comments