DONALD Trump (70) amechaguliwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani.
Mfanyabiashara huyo amemshinda mshindani wake mkuu, Hillary Clinton (69).
Trump ameahidi kuwa Rais wa Wamarekani wote.

“Ninawaahidi sitawaangusha” amesema Trump.
Clinton amempigia simu Trump kukubali matokeo.
“Sasa ni wakati wa Marekani kutibu mareraha ya mgawanyiko”amesema Rais huyo mteule, Trump.
“Ninaahidi kwa kila raia wa nchi hii kwamba nitakuwa Rais wa wamarekani wote, na hili ni jambo muhimu sana kwangu” amesema Trump.
“Kwa ambao hawakuniunga mkono huko nyuma, na walikuwa wachache, nakuja kwenu mnisaidie na mnielekeze ili tufanye kazi pamoja na kuiunganisha nchi yetu”amesema na kukiri kwamba, uchaguzi ulikuwa mgumu.