Waziri mkuu mstaafu wa ufaransa Francois Fillon, anaongoza kwa ushindi katika mzunguko wa kwanza wa mchujo wa mgombea Urais katika chama cha mrengo wa kulia cha Republicans.

Kwa zaidi ya robo tatu ya kura zilizohesabiwa Fillon anamtangulia waziri mstaafu Alain Juppe, na Rais wa zamani Nicholous Sarkozy aliyemaliza muda wake ambaye ameshikilia nafasi ya tatu.
Sarkozy amekubali kushindwa na ameahidi kumpigia kura Fillon katika mpambano unaofuata siku ya Jumapili.
Yeyote atakayeshinda, atakuwa Rais wa Ufaransa kwa kumshinda mrengo wa kulia Bi Marine Le Pen mwenye msimamo wa kijamaa.