Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 21, 2016

Zaidi ya watu 100 wafariki kwenye ajali ya treni India

Idadi ya watu waliyofariki kutokana na ajali ya treni iliyotokea mapema leo kaskazini mwa India, imeongezeka na kupita watu 100 na kuwajeruhi mamia ya wengine.
Treni hiyo ilikuwa ikitoka Indore kuelekea Patna kabla ya kupoteza muelekeo na kutoka katika barabara ya reli na kuanguka ilipokaribia mji wa Mashariki wa Kanpur katika jimbo la Utter Pradesh.Maafisa wa kutoa huduma za dharura wanajaribu kuwaokoa manusura waliokwama katika mabehewa yaliyoanguka.
Waziri wa uchukuzi wa India ameamuru kufanywa kwa uchunguzi kubaini kilichosababisha ajali hiyo

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP