Urusi imeanzisha operesheni kubwa ya kijeshi nchini Syria kwa kutumia manowari na vikosi vya majini kuzizingira fukwe za nchi hiyo. Waziri wa ulinzi wa Urusi amesema kwamba kwa mara ya kwanza ndege za kivita zilitumika huku makombora ya meli yakirushwa kutoka meli nyingine.

Amesema kuwa mashambulizi hayo yaliwalenga kundi la Islamic State na waasi wenye uhusiano na Al Qaeda katika majimbo la Idlib na Homs.
Wakati huo huo mashambulizi ya anga ya jeshi la Syria yameendelea katika maeneo ya mashariki mwa Aleppo yanayodhibitiwa na waasi baada ya kusitishwa kwa wiki tatu.
Wanaharakati wanasema watu watano wameuwawa.Kwa upande mwingine Rais Putin amemfukuza kazi waziri wake wa maendeleo ya kiuchumi,Alexie Ulyukayev, ambaye anashtakiwa kwa kupokea hongo ya dola milioni mbili. Msemaji wa rais Putin Dimitri Pescov amesema rais hana imani tena na bwana Ulyukayev ambaye amekana mashtaka hayo.
Ulyukayev amekuwa waziri wa kwanza kukamatwa katika robo karne . Waziri mkuu, Dmity Medvedev ,analielezea tukio hilo kuwa ni tukio gumu kwa serikali yake ambalo ameshindwa kulielewa .
Bwana Ulyukayev anatuhumiwa kwa kuomba hongo ya dola milioni mbili ikiwa ni gharama ya kuthibitisha kampuni kubwa ya mafuta ya Rosneft ununuzi wa wadau kwa asilimia hamsini wa mpinzani wake kibiashara jambo lililoibua sintofahamu .