UGANDA: Aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya FDC, Dkt Kizza Besigye ameingia kwenye mtifuano mpya na Jeshi la Polisi la nchi hiyo baada ya askari hao kuweka vizuzi kwenye njia ya kuingia nyumbani kwa kiongozi huyo, katika kijiji cha Kasangati, wilaya ya Wakiso nje kidogo mwa Jiji la Kampala ili kuzuia wageni wasiende kumtembelea.

Katika mtifuano huo, Besigye alikamatwa na kuingizwa kwenye gari lapolisi huku wapambe wake nao wakikinukisha kumtetea kiongozi wao huyo.
Besigye aliwekwa kizuizini tangu alipojitangaza kuwa ameshinda urais kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika February, 18, 2016.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Uganda, Museveni alishinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 61 ya kura huku Besigye akipata asilimia 35.