Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ametangaza baraza jipya la mawaziri wakati nchi hiyo inakumbwa na maandamano ambayo yamesababisha kutangazwa kwa hali ya hatari.
Bwana Hailemarian amewateua mawaziri 21 wakiwemo wengine wapya kabisa kusimamia wizara za fedha na mambo ya nchi za kigeni.
Mtandao wa Twitter wa serikali umetangaza kuwa bunge limeidhinisha baraza hilo jipya la mawaziri.
Wengi wanayaona mabadiliko haya kama hatua dhidi ya misururu ya maandamano ambayo yalisababishaa kutangazwa kwa hali ya hatari mwezi uliopita.
Aliwaachisha kazi badhi ya washirika wake wakuu wakiwemo mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni na fedha.

Hali ya hatari ilitangazwa nchini Ethiopia kufuatia misururu ya maandamano
Image captionHali ya hatari ilitangazwa nchini Ethiopia kufuatia misururu ya maandamano

Kuondolewa kwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Tedros Adhanom, halikuwa jambo la kushangaza kuwa tayari amependekezwa na bara la Afrika kuwania uongozi wa shirika la afya dunia.
Mahala pake pamechukuliwa na kiongozi wa chama cha Oromo People's Democratic Organizationa ambao ni sehemu ya muungano unaoongoza.
Waziri wa ulinzi Siraj Fegessa ambaye anasimamia hali hiyo ya hatari amesalia na wadhifa wake.