Tetemeko kubwa la ardhi limeua watu zaidi ya 24 na kusababisha uharibifu mkubwa katika mkoa wa Aceh nchini Indonesia.
Maafisa wanasema watu wengi wamefukiwa kwenye vifusi vya majumba yaliyoporomoka.
Tetemeko hilo la nguvu ya 6.4 kwenye vipimo vya Richter lilitokea karibu na mji wa Sigli katika kisiwa cha Sumatra ambapo majumba mengi yameporomoka.
Shirika la utabiri wa hali ya hewa la Indonesia limesema hakuna hatari ya kutokea kwa kimbunga.
Mwaka 2004, mkoa wa Aceh uliathiriwa sana na kimbunga kilichosababishwa na tetemeko kubwa baharini. Watu 120,000 waliuawa mkoani humo.
Taasisi ya Jiolojia ya Marekani imesema tetemeko hilo lilitokea karibu na pwani mwendo wa saa 11:03 asubuhi saa za huko (22:03 GMT Jumanne) katika kina cha 17.2km (maili 11) chini ya ardhi.
Said Mulyadi, naibu mkuu wa wilaya ya Pidie Jaya, eneo lililoathiriwa pakubwa na tetemeko hilo, ameambia idhaa ya BBC ya Indonesia kwamba huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.
Maafisa wamesema huenda kusitokee kimbungaImage copyrightAFP
Image captionMaafisa wamesema huenda kusitokee kimbunga
Map of Indonesia
Vifusi vya jumba mkoani Aceh tarehe 7 Desemba 2016.Image copyrightAFP
Image captionMaafisa wa uokoaji wanawatafuta manusura
Vifusi vya jumba Pidie, Indonesia Sumatra, Desemba 7, 2016.Image copyrightAFP/GETTY IMAGES
Image captionMaafisa wanahofia huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka kwani watu wengi wamefukiwa kwenye vifusi vya majumba yaliyobomoka